Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makumi ya watu wafariki katika ajali nyingine ya boti DRC

Makumi Ya Watu Wafariki Katika Ajali Nyingine Ya Boti DRC Makumi ya watu wafariki katika ajali nyingine ya boti DRC

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Takriban watu 40 wamekufa maji baada ya boti ya abiria kupinduka kwenye mto magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wiki moja baada ya wengine 47 kufariki katika ajali sawa na hiyo.

Boti hiyo ya mbao, inayojulikana kwa jina la nyangumi, ilikuwa imebeba abiria na mizigo, ilipopinduka kwenye mto Lulonga Jumamosi usiku.

Tukio hilo lilitokea karibu na kijiji cha Boyeka katika jimbo la Equateur.

Abiria hao, wengi wao wakiwa wafanyabiashara, walikuwa wakirejea kutoka katika soko la ndani kuelekea Mbandaka, mji mkuu wa jimbo hilo.

Idadi ya vifo huenda ikaongezeka huku abiria zaidi wakiripotiwa kupotea.Zaidi ya wengine 200 walinusurika, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Ajali hiyo imekuja siku kumi baada ya boti nyingine kupinduka katika jimbo hilo hilo na kusababisha vifo vya watu kadhaa na idadi na idadi isiyojulikana ya wengine hawajulikani walipo.

Maboti hutumiwa kama usafiri wa kawaida nchini Congo kwa sababu ya ukosefu wa barabara.

Hata hivyo, ajali za boti hutokea mara kwa mara kwa sababu ya mizigo mingi, kutokarabatiwa na kusafiri usiku.

Chanzo: Bbc