Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makumi ya watu wafariki baada ya basi kutumbukia mtoni nchini Mali

Makumi Ya Watu Wafariki Baada Ya Basi Kutumbukia Mtoni Nchini Mali Makumi ya watu wafariki baada ya basi kutumbukia mtoni nchini Mali

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Watu 31 wamefariki baada ya basi kutumbukia mtoni nchini Mali siku ya Jumanne.

Basi hilo lilikuwa likielekea nchi jirani ya Burkina Faso kutoka mji wa Kenieba nchini Mali wakati lilipoanguka kutoka kwenye daraja la mto Bagoe.

Watu kumi walijeruhiwa - baadhi yao wakipata majeraha mabaya.

Maafisa wa eneo hilo walisema huenda ajali hiyo ilitokana na "dereva kushindwa dereva kulidhibiti gari".

Ajali hiyo ilitokea mwendo wa 17:00 saa za ndani (17:00 GMT).

"Basi... lililokuwa likitoka wilaya ya Kenieba kuelekea Burkina Faso lilipoanguka kutoka kwenye daraja.

Sababu inayowezekana ni dereva kupoteza udhibiti wa gari," wizara ya uchukuzi ilisema katika taarifa.

Imeongeza kuwa waathiriwa ni pamoja na raia wa Mali na raia kutoka maeneo mengine ya Afrika Magharibi.

Ajali za barabarani hutokea mara kwa mara nchini Mali kwa sababu ya miundo misingi duni ya barabara na magari yasiyo katika hali nzuri ambayo hubeba mizigo kupita kiasi.

Mapema mwezi huu, watu 15 walifariki na 46 kujeruhiwa baada ya basi lililokuwa likielekea mji mkuu Bamako kugongana na lori, kulingana na shirika la habari la AFP.

Chanzo: Bbc