Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makumi ya watu wafa maji baada ya mashua kuzama Senegal

Makumi Ya Watu Wafa Maji Baada Ya Mashua Kuzama Senegal.png Makumi ya watu wafa maji baada ya mashua kuzama Senegal

Wed, 11 Sep 2024 Chanzo: Bbc

Takriban watu 26 wamefariki dunia baada ya mashua iliyokuwa imebeba wahamiaji kupinduka katika pwani ya Senegal.

Mamlaka zinasema zaidi ya watu 100 walikuwa kwenye mashua hiyo ya mbao wakati ilipozama kilomita 4 tu tangu kuanza safari yake.

Ndugu na marafiki waliofadhaika wamekusanyika kando ya ufuo huo, wakingojea kwa hamu habari za wapendwa wao.

Kufikia sasa, watu wanne wameokolewa na juhudi za kuwatafuta wale ambao hawajulikani walipo bado zinaendelea.

Boti hiyo ilikuwa imeondoka Mbour, takriban kilomita 80 kusini mwa mji mkuu Dakar, kuelekea Visiwa vya Canary vya Uhispania, ambavyo viko nje ya pwani ya Afrika Magharibi.

Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya wahamiaji wanaoondoka Afrika Magharibi kupitia Senegal imeongezeka.

Vijana wengi - wanaokimbia migogoro, umaskini, na ukosefu wa ajira - wanajaribu njia hatari ya Atlantiki kuelekea Visiwa vya Uhispania, huku karibu watu 30,000 wakirekodiwa kufika eneo hilo mwaka huu.

Chanzo: Bbc