Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makumi watiwa nguvuni Sierra Leone kuhusiana na jaribio la mapinduzi

Sierra Leone Mapinduzi Mbaroni Makumi watiwa nguvuni Sierra Leone kuhusiana na jaribio la mapinduzi

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Sierra Leone imetangaza kuwa watu wengine 43 wametiwa nguvuni kwa tuhuma za kuhusika na jaribio la mapinduzi la Novemba 26, na hivyo kufanya idadi ya watu waliokamatwa kufikia 57, wengi wao wakiwa wanajeshi.

"Watu 57 wamekamatwa tangu baada ya jaribio lililoshindwa, ikiwa ni pamoja na 43 mwishoni mwa wiki iliyopita", amesema Naibu Waziri mwenye dhamana ya habari, Yusuf Keketoma Sandi, bila kutaja eneo na mazingira ya kukamatwa kwao.

Sandi amesema, watu hawa 57 ni askari 37, raia 10, askari wanne waliofukuzwa jeshini, maafisa watano wa polisi na mstaafu mmoja. Hata hivyo hajaweka wazi majina ya viongozi wa jaribio hilo la mapinduzi.

Jumamosi iliyopita Rais wa Sierra Leone, Julius Maada Bio aliahidi kwamba jibu la serikalii kwa matukio hayo litachochewa na "kuheshimu sheria". Rais Julius Maada Bio

Mapema Novemba 26, wanajeshi waliokuwa na silaha walishambulia ghala la jeshi, kambi mbili, magereza mawili na vituo viwili vya polisi, na kukabiliana na vikosi vya usalama kwa mtutu wa bunduki.

Mapigano hayo yalisababisha vifo vya watu 21 wakiwemo wanajeshi 14, afisa wa polisi, mlinzi wa magereza na washambuliaji watatu.

Hali ya kisiasa katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika imeendelea kuwa ya wasiwasi tangu kuchaguliwa tena kwa Rais Julius Maada Bio katika uchaguzi uliopingwa na mgombea mkuu wa upinzani mwezi Juni mwaka huu.

Ghasia hizo za Sierra Leone zinafuatia wimbi la mapinduzi ya kijeshi yaliyoshuhudiwa katika eneo hilo la Afrika Magharibi. Mapinduzi 8 ya kijeshi yameshuhudiwa katika maeneo ya Afrika Magharibi na Kati tokea mwaka 2020, yakiwemo mapinduzi ya Mali, Burkina Faso, Niger na Guinea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live