Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makubaliano ya kusitisha mapigano yarefushwa DR Congo

Makubaliano Ya Kusitisha Mapigano Yarefushwa DR Congo.png Makubaliano ya kusitisha mapigano yarefushwa DR Congo

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Marekani imesema makubaliano ya kusitisha mapigano ili misaada ya kibinadamu iweze kufikishwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamerefushwa kwa siku kumi na tano zijazo hadi mapema mwezi Agosti.

Marekani imesema inafurahishwa na uamuzi huo wa kusitishwa mapigano.

Mashirika ya kutoa misaada Congo yameitaja hali ya kibinadamu mashariki mwa nchi hiyo kuwa janga na kuonya huenda mzozo wa Congo ukasambaa na kuziathiri pia nchi jirani.

Uasi wa kundi la M23 katika jimbo la Kivu Kaskazini umesababisha zaidi ya watu milioni tatu kuachwa bila ya makazi.

Chanzo: Bbc