Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makovu ya manusra wa ajali yamemfanya bingwa wa kuunda baiskeli za umeme

079fdeecab52582e Makovu ya manusra wa ajali yamemfanya bingwa wa kuunda baiskeli za umeme

Sun, 24 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Baada ya Wamae kujeruhiwa katika ajali, aliamua kuwajali wale ambao walikuwa na ulemavu

- Mjasiriamali huyo aliyefika tu kidato cha nne alikuwa akitengeneza baiskeli ya miguu tatu lakini baadaye akaamua kuunda viti vya magurudumu vinavyotumia umeme

- Watu wachache wanaoishi na ulemavu wamefaidika na ubunifu na bidii ya Wame mwenye umri wa miaka 34

Lincoln Wamae ni Mkenya ambaye kwa ujuzi wa kuzaliwa anasaidia kuondoa shida zinazowakumba walemavu kwa kutumia vitu vilivyotupwa. Anaunda baiskeli maalumu kwa ajili ya Wakenya walemavu.

Mnamo 2019, aliiambia BBC kuwa, alianza kutengeneza viti vya umeme kwa kutumia vyuma vikuukuu baada ya ajali iliyomwacha na majraha. Kwake, ilianza tu kama uraibu na baadaye ikawa kazi ailiyoifanya kwa moyo wake wote.

Lincoln, 34, alitumia miaka mitatu kuupiga msasa muundo wa kiti chake cha umeme kwa kutumia betri zilizotumika kwenye vipakatalishi na vitu vingine alivyopata kutoka katika majaa ya taka.



Tofauti na wajasiriamali wenye ujuzi mwingi kutoka Afrika, yeye hakusomea hata kidogo. “Siri ni kujaribu tu,” alisema wakati anahojiwa.

Kitu alichopenda na kuanza kufanya kwa moyo wake wote sasa ni biashara. Alitengeneza viti hivyo vya magurudumu hadi alipoona haja ya kuwaondolea taabu walemavu. Hapo ndipo alipoamua kubadilisha baiskeli yake ya miguu mitatu kuwa kiti cha magurudumu kinachotumia umeme.

Aliunda kiti chake cha kwanza cha magurudumu kinachotumia umeme mnamo Disemba 2018 na tangu hapo ameunda vingi zaidi. Akipewa vifaa vyote anavyohitaji, Lincoln anasema itamchukua siku moja kuunda kiti chenye magurudumu.

Haundi tu viti hivi kwa kutumia vifaa chakavu ambavyo hukusanya kutoka kwenye maeneo ya kutupa vyuma kuukuu; bali pia anaokoa mazingira.

“Viti vyangu vya magurudumu vinaendeshwa na betri za lithiamu-ion. Nazipata kwenye betri za zamani za vipakatalishi. Katika mchakato huo ninaokoa mazingira kwa sababu ninatumia taka-za kielektroniki," Lincoln alifichua.

Mzinduzi huyo wa kujigundulia mwenyewe amekuwa akitarajia kuunda kwa wingi ubunifu wake siku zijazo na kuuza kote Afrika.

Mchango wake Raphael Abuna, Mwalimu Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Igunga

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke