Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makamanda wa majeshi ya nchi za SADC, DRC, Burundi wakutana

Makamanda Wa Majeshi Ya Nchi Za SADC, DRC, Burundi Wakutana Makamanda wa majeshi ya nchi za SADC, DRC, Burundi wakutana

Fri, 1 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Makamanda wa majeshi ya nchi za SADC RDC na Burundi wamekutana mjini Goma Mkuu wa Jeshi la Afrika Kusini Jenerali Rudzani Maphwanya alipokelewa Alhamisi mjini Goma Makamanda wa majeshi ya Afrika Kusini, Malawi, Tanzania na Burundi wamewasili katika mji wa Goma kwa ajili ya mkutano, kulingana na msemaji wa jeshi la DRC.

Afrika Kusini, Malawi na Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Afrika SADC ambazo zimetuma wanajeshi na vifaa kusaidia vikosi vya serikali mjini Kinshasa dhidi ya kundi la M23.

Wanajeshi wa Burundi pia wanasemekana kusaidia vikosi vya serikali ya Congo katika mzozo huu, ingawa mamlaka ya Gitega imekuwa ikikanusha.

Kanali Guillaume Ndike Kaiko, msemaji wa utawala wa kijeshi wa Mkoa wa Kivu Kaskazini, ameiambia BBC kwamba makamanda wa kijeshi wa nchi hizo walifika Goma siku ya Alhamisi lakini alipoulizwa mkutano huo utajadili nini alijibu ‘’[Hebu] tusubiri”.

Shirika la habari la Congo linasema kuwa wa kwanza kuwasili Goma siku ya Alhamisi alikuwa mkuu wa jeshi la Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda na ujumbe wa mkuu wa jeshi la Malawi.

Wengine waliofika Goma ni Jenerali Christian Tshiwewe, Kamanda Mkuu wa Jeshi la RDC, Mkuu wa Jeshi la Afrika Kusini Jenerali Rudzani Maphwanya na Jenerali Prime Niyongabo na Kamanda wa Jeshi la Burundi, kwa mujibu wa shirika la habari la Congo.

Chanzo: Bbc