Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makaburi yaliyofungwa miaka 127 yafunguliwa!

Makaburi Sa Sa.jpeg Makaburi yaliyofungwa miaka 127 yafunguliwa!

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makaburi ya kihistoria ya Waislamu yanayopatikana katika barabara ya Brodie huko Wynberg katika mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini yamefunguliwa tena baada ya kupita miaka 127.

Nyaraka za kihistoria zinaonyesha kuwa serikali ya wakati huo ya kikoloni nchini Afrika Kusini iligawa ardhi hiyo ya eneo la makaburi kwa jamii ya Waislamu mwaka 1848. Mazishi ya mwisho kufanyika katika makaburi hayo yalikuwa mnamo mwaka 1896.

Katika taarifa yake, Kamati ya Msikiti wa Yusufeyyah na Baraza la Sheria la Waislamu (MJC) zimetangaza kuwa eneo hilo la makaburi ya Waislamu limefunguliwa tokea siku ya Ijumaa na kwamba shughuli za mazishi zimeruhusiwa kufanyika kuanzia siku ya Jumamosi na kuendelea.

Imam Badrodien ambaye anafahamika kama kiongozi wa eneo la Wynberg ndiye aliyekabidhiwa uangalizi wa makaburi hayo kwa niaba ya jumuiya ya Waislamu wa Wynberg. Baraza la Sheria la Waislamu ambalo limeshirikiana kwa karibu na upande unaosimamia makaburi hayo limekaribisha kufunguliwa tena eneo hilo la makaburi ya kihistoria ya Waislamu huko Cape Town.

Wakati huo huo, Sheikh Riad Fataar Mwenyekiti wa idara inayosimamia mazishi ya Baraza la Sheria la Waislamu (MJC) ameeleza na hapa ninamnukuu" tutafanya kazi, tunajaribu kuokoa fedha za jiji. Tutatatunza makaburi haya, tutasimamia usalama na mambo yote mengine," mwisho wa kunukuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live