Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majirani wa Naibu wa Rais Kenya walalamikia kelele nyumbani kwake

68629 Pic+ruto Majirani wa Naibu wa Rais Kenya walalamikia kelele nyumbani kwake

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: BBC

Wakazi wa maeneo ya kifahari jijjini Nairobi nchini Kenya wamemuandikia Naibu Rais wa taifa hilo na kulalamikia kuhusu kelele zinazotoka nyumbani kwake.

Makamu wa rais William Ruto amekuwa akifanya mikutano ya kisiasa nyumbani kwake huko Karen.

Wakazi sasa wanasema kwamba kelele kutoka mikutano hiyo ya kisiasa zinawadhuru.

Pia wamelalamikia kuhusu usalama wao , ikiwemo wizi wa mabavukatika barabara inayoelekea katika nhyumba ya kiongozi huyo na watu wanaojifanya kuwa wageni wa nyumba hiyo ya makamu wa rais, alisema mwenyekiti wa Muungano wa wakaazi wa eneo hilo James Hirst.

Wageni walioegesha magari yao nje pia wameshtumiwa kwa kusababisha trafiki katika njia hiyo. Familia Tajiri huishi katika eneo la Karen ambapo kuna usalama wa saa 24.

Chanzo: BBC