Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majibu ya Rais Kenyatta baada ya kutajwa kwenye kashfa ya “Pandora Papers”

KENYATTA PANDORA Majibu ya Rais Kenyatta baada ya kutajwa kwenye kashfa ya “Pandora Papers”

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amejibu ripoti ya ya ufichuaji nyaraka za siri kuhusu mali za siri za viongozi wakubwa kutoka nchi mbalimbali zilizochapishwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Uandishi wa Habari za Upelelezi (ICIJ).

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, Rais Kenyatta amesema ripoti hiyo ambayo imegusa utajiri wa familia yake na viongozi wengine wa ulimwengu, itasaidia sana katika kuongeza taarifa za kifedha na uwazi nchini Kenya na kote ulimwenguni.

"Usafirishaji wa fedha haramu, mapato ya uhalifu na ufisadi hustawi katika mazingira ya usiri na giza," Amesema Kenyatta.

Alidokeza pia kwamba ufuatiliaji wa ukaguzi huo wa kifedha utasaidia kugundua utajiri ambao hauelezeki.

"Karatasi za Pandora na ukaguzi wa baadae utafuatilia pazia hilo la usiri na giza kwa wale ambao hawawezi kuelezea mali zao au utajiri", Rais Kenyatta alisema.

Walakini, taarifa hiyo haikushughulikia madai maalum yaliyotolewa katika ripoti hizo kulingana na Karatasi za Pandora.

Amesema ataijibu kikamilifu atakaporudi kutoka kwenye ziara yake nchini Marekani.

Kupitia ripoti ya Pandora, makumi ya viongozi wa mataifa mbalimbali ikiwemo Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair wametajwa katika ripoti zinazoonesha biashara za siri na malipo ya pesa yasiyoelezeka.

Mbali na Kenyatta, wengine waliotajwa ni pamoja na Mfalme Abdullah II wa Yordani, Waziri Mkuu wa Czech Andrej Babis, mwimbaji wa nyimbo wa Colombia Shakira na supermodel wa Ujerumani Claudia Schiffer.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live