Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeshi yaondoka nyumbani kwa Bob Wine

A0617aad300e762651530723d0e90ba3 Majeshi yaondoka nyumbani kwa Bob Wine

Thu, 28 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Vikosi vya majeshi ya Uganda vimeondoka kwenye makazi ya kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu ‘Bobi Wine’ baada ya Mahakama nchini humo kuamuru kufanya hivyo siku tatu zilizopita.

Majeshi hayo yalikua yamezingira nyumba ya ‘Bob Wine’ na kumuweka kizuizini tangu Januari 14,2020.

Vikosi hivyo vya usalama viliweka kambi nyumbani kwa Bobi ‘Wine’ mara baada ya uchaguzi kwa kile walichodai kuwa ni kumlinda.

Uchaguzi huo mkuu wa Uganda, ulimpa ushindi Rais Yoweri Museveni, matokeo ambayo yamepingwa na ‘Bob Wine’ akidai kuwa uligubikwa na udanganyifu.

Chanzo: habarileo.co.tz