Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeshi ya anga ya Morocco na Israel yafikia makubaliano

Makubalianoooooooo Majeshi ya anga ya Morocco na Israel yafikia makubaliano

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamada wa jeshi la utawala haramu wa Isarel amefanya safari nchini Morocco katika kipindi hiki ambacho wananchi wa nchi hiyo wameendelea kulalamikia hatua ya Rabat ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu.

Katika safari hiyo Jenerali Tomer Bar amekutana na kufanya mazungumzo na Kamanda wa jeshi la Anga la Morocco Jenerali El-Abed Alaoui Bouhamid ambapo wawili hao wamefikia makubaliano ya kuwa na ushirikiano katika masuala ya anga.

Aidha ujumbe wa kijeshi wa Israel ulioongozwa katika safari hiyo ya Morocco na kamanda wa jeshi la utawala huo ghasibu pamoja na mambo mengine ulitembelea kambi ya jeshi la anga la Morocco na Chuo Kikuu cha Kikosi cha Anga. Morocco na Israel zimefikia makubaliano pia ya kufanya luteka ya pamoja ya kijeshi ya anga.

Desemba 2020, Morocco na utawala haramu wa Israel zilifikia mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida kwa ushawishi wa Marekani. Na kama sehemu ya makubaliano hayo, Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump alikubali kutambua mamlaka ya Morocco juu ya Sahara Magharibi. Hata hivyo serikali ya rais wa sasa wa nchi hiyo Joe Biden imesema itauangalia upya uamuzi huo.

Nchini Morocco, kuwa na uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel ni maudhui nyeti inayogusa na kutonesha hisia za Wamorocco waliowengi ambao wanawaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina, kama ilivyodhihirishwa na wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya nchi hiyo walionyanyua bendera ya Palestina mara kadhaa wakati wa mashindano ya mara hii ya Kombe la Dunia yaliyofanyika nchini Qatar kuonyesha mshikamano na taifa hilo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live