Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majeneza 150 yateketea kwa moto

Jeneza FPA2XXI4WG2UY Majeneza 150 yateketea kwa moto

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majeneza 150 yaliyokuwa yametengenezwa kwa ajili ya biashara yameteketea kwa moto katika mjiwa Karatina, uliopo eneo la Bunge Mathira Nchini Kenya.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,wamesema mbali na Majeneza hayo,pia Samani nyingine ikiwemo Meza,Viti na Makabati vimeteketea kwa moto huo unaodaiwa kuwa mkubwa uliotokea katika mtaa wa Sofia.

Kamishna wa Nyeri, Peter Murugu amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na kwamba uliripotiwa kutokea majira ya saa tisa alasiri na kuleta uharibufu katika Maduka ya juakali, yaliyoko mtaa huo wa Sofia.

Amesema,uchunguzi wa awali ulifanywa kikamilifu ulibaini kiwango cha hasara ambapo alisema kuwa ni mamilioni ya fedha

Naye mmoja wa waathiriwa, James Njogu amesema amepoteza majeneza 16 aliyokuwa ameweka katika duka lake akisubiri wateja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live