Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majangili waua wanajeshi wawili wa KDF, 7 wako Nairobi kwa matibabu

D0b2a3066019f7e3 Majangili waua wanajeshi wawili wa KDF, 7 wakimbizwa Nairobi kwa matibabu

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wanajeshi Saba (KDF) wamesafirishwa kwa ndege kwa matibabu ya dharura Nairobi baada ya kuvamiwa kazini na majangili wenye silaha mnamo Jumatano, Novemba jana November 10.

Helikopta ya kijeshi iliwachukua maafisa saba waliojeruhiwa kutoka eneo la vita baada ya kikosi cha maaskari zaidi kutumwa kuwaokoaWanajeshi hao walikuwa wakichimba mtaro kando ya Hifadhi ya Mazingira ya Laikipia (LNC) ili kuwazuia majambazi kutoka katika eneo hilo na kuvamia vijiji jirani.

Duru zinaarifu kwamba wahalifu hao waliharibu mashine za ujenzi wakati wa ufyatulianaji risasi lakini walishindwa kutoroka na bunduki walizokuwa wakilenga kuiba

Wenzao wawili walifariki dunia papo hapo baada ya majambazi kuwalaza katika eneo la Kamwenje, Laikipia Magharibi.

Helikopta ya kijeshi iliwachukua maafisa saba waliojeruhiwa kutoka eneo la vita baada ya kikosi cha maaskari zaidi kutumwa kuwaokoa.

Wanajeshi hao walikuwa wakichimba mtaro kando ya Hifadhi ya Mazingira ya Laikipia (LNC) ili kuwazuia majambazi kutoka katika eneo hilo na kuvamia vijiji jirani.

Duru zinaarifu kwamba wahalifu hao waliharibu mashine za ujenzi wakati wa ufyatulianaji risasi lakini walishindwa kutoroka na bunduki walizokuwa wakilenga kuiba.

TUKO.co.ke iliripoti kuwa polisi watatu walifariki dunia huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya katika kisa cha ufyatulianaji risasi na majambazi katika maeneo ya Hifadhi ya Mazingira ya Laikipia mnamo Jumatano, Oktoba 27.

Tukio hilo lililoripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Ol Moran, lilitokea wakati askari hao walipovamiwa na majambazi.

Polisi hao ambao wako chini ya kikosi cha maafisa wa mashirika mengi wanaendelea kuwatimua majambazi katika eneo hilo ili kurejesha hali ya utulivu.

"Hifadhi ya Mazingira iko chini ya ulinzi wa mashirika mengi, na wenyeji wanaombwa kusalia watulivu," taarifa ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi ilisema.

Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i aliunda kikosi cha mashirika mengi ambayo yanajumuisha maafisa kutoka Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS), vitengo vya doria mpakani na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), katika harakati za kuleta amani katika eneo hilo.

Mapema mwezi huu, Oktoba 13, 2021, Waziri Mkuu alibainisha kwa wasiwasi mkubwa kwamba majambazi walikuwa wameendelea kutawala wakazi licha ya juhudi za kudumisha amani.

"Majambazi hatari wanaendelea kunufaika na hali ukame uliopo katika kaunti jirani," akasema.

Serikali ilifichua kuwa majambazi walikuwa wamebuni njia mpya za kufanya uvamizi wa uhalifu kama vile kujifanya kuwa wafugaji.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke