Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Majambazi' zaidi ya mia moja wauawa katika mashambulizi ya anga Nigeria

D99D3742 AED0 4A3A BDEA 20AA05E90F67.jpeg 'Majambazi' zaidi ya mia moja wauawa katika mashambulizi ya anga nchini Nigeria

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa siku ya Jumanne na jeshi la Nigeria yalisababisha vifo vya takriban majambazi zaidi ya mia moja wa kundi la wahalifu wenye silaha kaskazini-magharibi mwa Nigeria, eneo lililokumbwa na ghasia zilizosababishwa na magenge ya "majambazi".

Jeshi la Wanahewa la Nigeria limethibitisha rasmi siku ya Ijumaa kuwa lilifanya mashambulizi ya anga katika jimbo la Zamfara lakini halikutoa maelezo kuhusu idadi ya watu waliouawa.

Maeneo ya kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria kwa miaka mingi yamekuwa yakikumbwa na ghasia kutoka kwa "majambazi" ambao huvamia vijiji vilivyotengwa ambako wanaua na kuwateka nyara wakazi kwa kuwakomboa kwa fidia, na kuchoma nyumba baada ya kuwapora.

"Ndege za kivita zilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya majambazi. Nina hakika zaidi ya mia moja waliuawa na karibu mara mbili ya idadi hiyo walijeruhiwa vibaya," afisa wa kijeshi aliyehusika katika operesheni hiyo ameliambia shirika la habari la AFP.

Kulingana na chanzo hiki, majambazi hao walikuwa wakikusanyika katika eneo linalozunguka majimbo ya Zamfara, Kebbi na Niger, kwa nia ya kushambulia baadhi ya vijiji na kambi ya kijeshi. Akihojiwa na shirika la habari la AFP, msemaji wa jeshi la wanahewa la Nigeria, Commodore Edward Gabkwet, amethibitishamashambulizi haya. "Lakini siwezi kuthibitisha takwimu," amesema.

Muungano kati ya majambazi na wanajihadi

Hii ni operesheni ya pili mbaya zaidi ya anga dhidi ya "majambazi" katika Jimbo la Zamfara tangu mwaka 2015, wakati jeshi lilipotumwa kupambana na magenge haya. Raia wawili wanaoishi karibu na eneo lililolipuliwa wamelithibitishia shirika la habari la AFP kwamba waliona zaidi ya maiti mia moja kwenye eneo la tukio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live