Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majambazi waua watu 37 Nigeria

E2B0A9D6 9246 4AB8 96C5 3F24E4DAA1AB.png Majambazi waua watu 37 katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majambazi nchini Nigeria wamewaua watu 37 katika mashambulizi mapya dhidi ya jamii Kaskazini Magharibi mwa jimbo la Kaduna.

Kwa mujibu wa taarifa, majambazi hao Jumapili usiku walishambulia jamii za Malagum na Sokwong za kitongoji cha Kagoro katika eneo la Kaura jimboni humo ambapo pia waliteketeza zaidi ya nyumba 100.

Shambulio hilo limetokea chini ya saa 48 baada ya Jeshi la Anga la Nigeria kuvamia pango la majambazi katika eneo hilo katika operesheni maalum na kuwaua wengi wao na kuwaokoa raia wa China waliokuwa wameshikiliwa mateka kwa muda wa miezi sita.

Spika wa Baraza la Kutunga Sheria la Serikali ya Mitaa ya Kaura, Bw Ahmed Abutu, alithibitisha Jumatatu kwamba majambazi hao walitekeleza mashambulizi hayo.

Kando na kuchoma nyumba hizo, pia waliharibu magari na pikipiki nyingi. Kulingana naye, nyumba zote za jamii ya Sokwong ziliharibiwa kabisa na majambazi hao huku eneo lote likiwa limeachwa bila watu.

Habari za shambulio hilo zimekatisha furaha iliyoibuka baada ya kuokolewa raia saba wa China waliotekwa nyara mwezi Juni.

Wakati huo huo, katika operesheni kali dhidi ya magaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria, makamanda wanne wakuu wa kundi la kigaidi la Boko Haram wamejisalimisha kwa wanajeshi wa Nigeria katika Jimbo la Borno.

Hayo yanajiri miezi michache baada ya vikosi vya majeshi ya Chad, Cameroon, Nigeria na Niger kufanya shambulio lililoratibiwa kwa pamoja na nchi hizo nne kwa lengo la kuliangamiza kundi la Boko Haram na makundi mengine ya kigaidi yanayoendesha harakati zao katika eneo la kandokando ya Ziwa Chad.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live