Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majambazi wanne wauawa na Polisi, mmoja atoroka

Image 411 1140x640.png Majambazi wanne wauawa na Polisi, mmoja atoroka

Wed, 14 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Maafisa wa Polisi kwa kushirikiana na wale wa Idara ya upelelezi – DCI, nchini Kenya wamewauwa kwa kuwapiga risasi washukiwa wanne wa ujambazi, katika eneo la Mkwajuni barabara kuu ya Mombasa Malindi.

Maafisa hao wamefanikisha mauaji hayo baada ya kuwafuatilia majambazi hao waliokuwa kwenye gari dogo wakitoka upande wa Mombasa, majira ya saa tisa alfajiri ya Juni 13, 2023, huku jambazi mmoja akitoroka.

Katika tukio hilo, Polisi walipata bunduki moja aina ya AK-47 inayodaiwa kuibwa kwenye tukio la uvamizi wa benki ya Equity, tawi la Matuu, Kaunti ya Machakos Julai 2021.

Hata hivyo, Polisi nchini humo inasema msako mkali unaendelea ili kuweza kumkamata jambazi aliyetoroka na kwamba zoezi hilo litaendela ili kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unakuwepo.

Chanzo: Dar24