Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majambazi Wenye Silaha Wavamia Benki ya Equity Kisumu

Majambazi Equit Majambazi Wenye Silaha Wavamia Benki ya Equity Kisumu

Tue, 23 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mjini Kisumu wanakabiliana na majambazi ambao wamevamia Benki ya Equity iliyo mtaa wa Ang'awa nchini Kenya, wakitaka kupora fedha mchana huu.

Washukiwa wanne wa ujambazi waliojihami kwa silaha kali wamevamia benki hiyo leo Jumanne, Novemba 23,  baada ya kujifanya wateja.

Baada ya kufika kwenye ukumbi wa benki hiyo, walirusha bomu la machozi, hali iliyowalazimisha baadhi ya wateja na wahudumu wa benki kukimbilia usalama wao.

Kikosi cha maafisa wa polisi kinaongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Nyanza, Karanja Muiruri ambapo bado wanapambana na majambazi hao kwa zaidi ya saa moja, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, ni sauti tu zimekuwa zikisikika ndani ya benki hiyo 'lala chini.'

Kikosi cha zimamoto nacho kimewasili haraka eneo hilo kusaidia kuokoa na kumwaga maji ili kupunguza makali ya bomu la machozi.

Wanafunzi wawili waliokuwa ndani ya benki hiyo kupata huduma ya kulipia ada zao za shule baada ya kurejea kutoka likizo, wamenusurika kufuatia risasi zilizopigwa kuwaparaza vichwani na kuwajeruhi, wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Wafanyakazi wengine wa benki hiyo wameokolewa na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu lakini hadi wakati wa kuchapisha taarifa hii, polisi walikuwa wameshindwa kuwakamata majambazi waliovamia Benki ya Equity tawi la Angawa huko Kisumu nchini Kenya. Polisi hao wamewachukua kila mtu aliyekuwa ndani ya benki hiyo kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live