Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majambazi Wavamia Makazi ya Jirani wa Mstaafu Rais Mwai Kibaki, Waiba KSh 20M

5398b4c846eb8af3 Majambazi Wavamia Makazi ya Jirani wa Mstaafu Rais Mwai Kibaki, Waiba KSh 20M

Wed, 9 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Genge la majambazi limeripotiwa kuvamia boma la jirani wa rais mstaafu Mwai Kibaki na kuiba KSh 20 milioni

- Hakuna majeruhi yalioripotiwa kwenye uvamizi huo, tayari maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kufuatia kisa hicho na wanawasaka majambazi hao

- Kabla wafanikiwe kuingia nyumbani kwa Harish Patel, waliwafunga walinzi pamoja na wafanyakazi wa nyumbani kwa kamba na kuwaonya dhidi ya kupiga nduru

Majambazi watatu wameripotiwa kuvamia makaazi ya kifahari ya jirani wa Rais mstaafu Mwai Kibaki mtaani Muthaiga usiku wa kuamkia Jumapili, Juni 6.

Kulingana na taarifa tulizozipokea hapa TUKO.co.ke, majambazi hao walifanikiwa kuiba KSh 20 milioni kutoka nyumbani kwa Harish Patel.

Patel ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Kenya Horticultural Export Limited.

Kwa mujibu wa taarifa za People Daily, majambazi hao waliruka uzio nakuweza kuingia bomani humo, waliwatishia wenyeji maisha kabla ya kuiba pesa hizo, hata hivyo hakuna yeyote aliyejeruhiwa.

Majambazi hao ambao waliwateka baaadhi ya wafanyakazi, waliwaamuru kuwaonyesha kulikuwa vyumba vya kulala wakiwa wamewashikia bunduki.

Maafisa wa polisi wakiongozwa na kamanda mkuu Julius Kiragu, majambazi hao hawakufyatua risasi wala kumjeruhi yeyote.

Patel ni jirani wa viongozi mashuhuri akiwemo aliyekuwa gavana wa Nairobi Evans Kidero, mfanyabiasha tajiri Manu Chandaria na balozi wa Uingereza humu nchini Jane Marriot.

Haya yanajiri miezi michache baada ya majambazi pia kuvamia makazi ya mfanyabiashaea Manu Chandaria na kuiba KSh600,000 na bidhaa zenye thamani.

Majmbazi hao wanasemekana kumpokonya afisa wa polisi wa kitengo cha utawala aliyekuwa akilinda makazi ya mfanyabiashara huyo na kutoweka na bunduki aina ya G3.

Afisa huyo pia alifungwa kwa kamba kabla ya kunyang'anywa bunduki.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke