Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaji wa Umoja wa Mataifa waamuru Félicien Kabuga aachiliwe huru

Majaji Wa Umoja Wa Mataifa Waamuru Majaji wa Umoja wa Mataifa waamuru Félicien Kabuga aachiliwe huru

Tue, 8 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Majaji wa Umoja wa Mataifa wameamuru kuwa mshukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Félicien Kabuga achukuliwe hatua za haraka za kuachiliwa huru na kwamba kesi ya uhalifu wa kivita dhidi yake isitishwe kwa muda usiojulikana.

Mwezi Juni, majaji katika mahakama ya uhalifu wa kivita ya Umoja wa Mataifa waliamua kuwa Bw Kabuga hafai kufikishwa mahakamani kutokana na ugonjwa wa akili lakini walipendekeza taratibu mbadala zifanyike. Kwa sasa majaji wa rufaa wamekataa pendekezo hili.

Kwa mujibu wa majaji, mahakama ya uhalifu wa kivita ya Umoja wa Mataifa ilifanya "kosa la sheria" mwezi Juni kwa kuamua kwamba Félicien Kabuga anapaswa kushitakiwa kupitia utaratibu mbadala uliorahisishwa licha ya hali yake ya afya. Na sasa mahakama ya mwanzo imeamrishwa kuhakikisha Bwe kabuga naachiliwa.

Mfanyabiashara huyo na mmiliki wa kituo cha redio, kilichotuhumiwa kuhamasisha mauji ya kimbari , ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 80, ni mmoja wa washukiwa wa mwisho waliosakwa na mahakama hiyo inayochunguza uhalifu uliofanywa wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Anatuhumiwa kueneza chuki na mauaji kupitia kituo chake cha redio na kuwahamasisha wauaji waliowaua zaidi ya watu 800,000 katika kipindi cha siku 100 tu. Alikamatwa mjini Paris mwaka 2020, baada ya miongo miwili ya kuwa mafichoni. Bw Kabuga alikanusha mashtaka.

Mahakama imekiri kuwa uamuzi huu wa hivi karibuni utawakatisha tamaa wahanga na manusura wa mauaji ya kimbari lakini imebainisha kuwa haki inaweza tu kutendeka kwa heshima kamili kwa haki za watuhumiwa.

Chanzo: Bbc
Related Articles: