Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaji 98 Wanawake Waapishwa Misri

91eb4d9f Aabd 4e1e 8130 64856cf79798 Majaji 98 Wanawake Waapishwa Misri

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

KWA mara ya kwanza katika historia, Misri imewaapisha  wanawake 98 kuwa Majaji katika moja ya vyombo vikuu vya idara ya mahakama nchini humo, inayofahamika kama Baraza  kuu la serikali.

Majaji hao waliapishwa mbele ya jaji mkuu wa baraza hilo katika hafla iliyofanyika katika mji mkuu Cairo jana  Jumanne, uapisho  huu unakuja miezi kadhaa baada Rais Abdul Fattah Al-Sisi kuwataka wanawake wajiunge na vyombo vikuu viwili vya mahakama, baraza na Mashtaka ya Umma.

Tangu kuanzishwa kwake mnamo 1946, baraza la serikali limekuwa likiwateua  wanaume pekee kuwa majaji na kukataa  maombi ya wanawake, katika miaka iliyopita, wanawake walipinga maamuzi ya baraza, hilo wakisema kuwa wanabaguliwa.

Chanzo: globalpublishers.co.tz