Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maisha ni magumu sana, asema Michael Njogo Gitonga anayefanana na Uhuru

Bc5020ce9d711782 Maisha ni magumu sana, asema Michael Njogo Gitonga anayefanana na Uhuru

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wengi walidhani picha za Michael Njogo Gitonga, baba ya watoto watatu ni za rais alipokuwa hajawa kiongozi wa taifa 2013Kulingana na Njogo sasa inambidi kuficha uso kutumia maski kwani ingawa kuna virusi vya corona vinavyofaa kudhibitiwa, maski inamsaidia kujificha ili asije kuangaliwa kila mara na watu wanaomfananaisha na Rais Uhuru KenyattaIngawa hana nguvu alizonazo rais wa Jamhuri ya Kenya, Njogo anafurahia umaarufu aliopata ambao umejiri na uzito fulani.Kwa mara ya kwanza jamaa anayefanana na Rais Uhuru Kenyatta amezungumza tangu picha zake zisambae mtandaoni na kuwafurahisha Wakenya.

Hakika, wengi walidhani picha za Michael Njogo Gitonga, baba ya watoto watatu ni za rais Uhuru alipokuwa hajawa kiongozi wa taifa 2013.

kama rais 2022



Ingawa hana nguvu alizonazo rais wa Jamhuri ya Kenya, Njogo anafurahia umaarufu aliopata ambao umejiri na uzito fulani.

“Siwezi kutembea mitaani kawaida bila ya watu kuniomba niwape kitu kidogo, napata taabu na jina hili,” alisema.

Njogo aliongeza: “Inanishangaza kiukweli, kwani najiuliza maswali ni kwa nini nafanana na Rais Kenyatta, si kitu cha kawaida,”

Wakati picha zake zilipokuwa sikisambaa mtandaoni, kuna baadhi ya watu waiodai labda picha hizo zilikuwa zimefanyika 'photoshop' huku wengine wakimtaka afanye Uchunguzi wa Asili nasaba (DNA) kuthibitisha ukweli wa mambo.

Polycarp litaitwa baba karibuni, mke wake anatarajia mtoto

Akiwa mwashi, kazi yake ya ufundi anasema hajakuwa akiifanya na kwamba baa yake mtaani Umoja biashara imedorora mno tangu zilipofungwa kutokana na janga la Covid-19.

Njogo anasema, anaamini na kutarajia siku moja ukweli utabainika kuhusu nani baba yake mzazi kwa kuwa mtu wa pekee anayefahamu kwa wazazi wake ni mama ambaye ni marehemu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke