Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maina Kamanda ajutia kampeni za chaguzi ndogo Nakuru na Naivasha mwezi Machi

8447c9eddb5c9cd1 Maina Kamanda ajutia kampeni za chaguzi ndogo Nakuru na Naivasha mwezi Machi

Wed, 14 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kamanda anasema aliugua maradhi ya Covid-19 wakati wa kampeni za wadi ya London na ile ya Hells Gate

- Maradhi hayo yalimkata mwili kwa kiasi kikubwa na kumfanya kuhofia kuwa yangemwangamiza

- Aliwataka Wakenya kuendelea kuzingatia sheria zilizowekwa na sekta ya afya katika kupambana na maambukizi ya janga hilo

Mwanasiasa Maina Kamanda amesimulia jinsi maradhi ya coronavirus yalimvamia na kumtesa kwa siku kadhaa huku akihofia huenda yakamzidi.

Kamanda alisema Covid-19 ilimuangukia wakati alipokuwa akishiriki kampeni za uchaguzi mdogo wa wadi ya London Nakuru na Hells Gate Niavasha mwezi Machi.

Alisema alichopitia ni hali ambayo hawezi taka kupitia tena kwani maumivu yalimkata mwili kwa kiasi kikubwa.

“Niliambukizwa wakati wa kampeni za chaguzi ndogo Nakuru na Naivasha," alisema Kamanda.

“Ilikuwa ni wakati huo ambapo Baba pia alitangaza ameambukizwa. Nililazwa hospitali na haikuwa mimi peke yangu. Ni wanasiasa wengi pia ambao waliugua lakini hawakutaka kujitokeza kusema hilo. Huu ugonjwa ni hatari sana," alisema Kamanda akiongea na redio ya Inooro.

Mbunge huyo wa Jubilee alishukuru Mungu kwa kuyaokoa maisha yake akisema alikuwa na matatizo makubwa ya kupumua.

"Niliyoyapitia yalikuwa ya kushtua sana. Ilifika wakati hata kupumua ilikuwa shida. Nashukuru Mungu kwa kuniponya," alisema Kamanda ambaye Wakenya wamekuwa wakiuliza alipo baada ya kupotea kwenye shughuli za umma.

Ugonjwa wa Covid-19 umekuwa tishio kubwa kwa taifa huku viongozi wengi wakiwa wameangamizwa.

Rais Uhuru Kenyatta alichukua hatua kali na kufunga kaunti za Nairobi, Nakuru, Kiambu, Machakos na Kajiado akisema idadi ya maradhi hayo ni ya juu.

Aidha alipiga marufuku pia mikutano yote ya siasa pamoja na maeneo ya ibada Jumapili katika kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari kemkem za TUKO

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke