Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yawaachilia washukiwa kesi ya Anglo leasing Kenya

Kortiniiii Mahakama yawaachilia washukiwa kesi ya Anglo leasing Kenya

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama ya kupambana na ufisadi imewaachilia washtakiwa wote waliohusishwa na kesi ya Anglo leasing ya Sh3.5 bilioni nchini Kenya .

Hakimu wa mahakama hiyo Martha Mutuku alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi ya awali dhidi ya washtakiwa wote.

“Wote wameachiwa huru chini ya kifungu cha 210 cha sheria ya makosa ya jinai, hawana kesi ya kujibu, wameachiwa huru,” alisema Hakimu Mashauri.

Katika kesi hiyo, familia ya Kamani pamoja na marehemu David Mworaria, aliyekuwa PS Dave Mwangi na Joseph Magari, David Onyonka, Sound Day Corporation na Apex Finance walishtakiwa kwa kutenda uhalifu wa kiuchumi.

Inadaiwa kuwa kati ya Oktoba 30, 2003, na Aprili 2004 wakiwa Nairobi, walipanga njama ya kushiriki katika njama ya kuilaghai serikali pesa hizo kupitia mkataba wa mkopo wa usambazaji wa vifaa vya kisasa vya Usalama wa Polisi.

Chanzo: Bbc