Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yatia hatiani boko haram 129

Boko Haram Naija.jpeg Mahakama yatia hatiani boko haram 129

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama nchini Nigeria imewatia hatiani wanamgambo 125 wa kundi la kigaidi la Boko Haram na wafadhili wa kifedha wa msururu wa makosa yanayohusiana na ugaidi.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Nigeria imesema mashtaka dhidi ya watu hao yalikuwa "yanahusiana na ugaidi, ufadhili wa ugaidi, kutoa msaada wa mali, na makosa ya jinai yaliyoainishwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC".

Kesi hiyo ya pamoja iliyosikilizwa kwa muda wa siku mbili iliendeshwa na majaji watano wa Mahakama Kuu ya Shirikisho katika kizuizi cha jeshi kwenye mji wa Kanji katika Jimbo la Niger.

Maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine wamelazimika kuhama makazi yao tangu ulipoanza uasi na mashambulio ya kundi la kigaidi la Boko Haram mwaka 2009. Mashambulio ya kundi hilo la ukufurishaji yamesababisha hali mbaya ya kibinadamu kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuifanya serikali ikabiliwe na mashinikizo ya kuitaka ikomeshe mgogoro huo.

Washtakiwa 85 kati ya 125 walitiwa hatiani kwa kufadhili ugaidi, 22 kwa makosa ya jinai yaliyoainishwa na ICC, na washtakiwa waliosalia walipatikana na hatia ya makosa ya ugaidi; na wote hao walihukumiwa vifungo tofauti.

Kesi za mwisho za watu walioshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram ziliendeshwa kati ya mwaka 2017 na 2018, ambapo watu 163 walipatikana na hatia na 887 waliachiliwa huru.

Mnamo mwaka wa 2014, kundi la kigaidi la Boko Haram liliwateka nyara wasichana zaidi ya 270 kutoka skuli moja ya mji wa kaskazini-mashariki wa Chibok.

Zaidi ya wasichana 180 wameachiliwa au kutoroka lakini wengine bado hawajulikani walipo.

Wale ambao wamerejea makwao, baadhi yao wakiwa wamaepata ujauzito na kujifungua wakiwa wanashikiliwa na Boko Haram, wanakabiliwa na matatizo mengi katika jamii zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live