Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaruhusu ndege kupeleka wahamiaji Rwanda

Rwanda Wakimbizi Ndege Mahakama yaruhusu ndege kupeleka wakimbizi Rwanda

Tue, 14 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndege ya kwanza ya serikali ya Uingereza inayowapeleka wa waombaji wa uhamiaji hadi Rwanda inaweza kufanya safari hiyo Jumanne, Majaji wa mahakama ya rufaa wamesema.

Mahakama hiyo imeunga mkono uamuazi uliotolewa awali na Mahakama ya juu nchini humo kwambani katika "maslahi ya umma" kwa serikali kutekeleza sera zake.

Chini ya mpango huo, baadhi ya wale wanaoingia nchini Uingereza kinyume cha sheria watasafirishwa kwa ndege hadi Rwanda ambako wataweza kutuma maombi ya uhamiaji wakiwa huko.

Wanaharakati walikuwa wakijaribu kuzuwia ndege kusafiri kabla ya kesi kamili kusikilizwa juu ya iwapo sera hiyo ni ya kisheria mwezi ujao.

Mapemamahakama iliambiwa kuwa watu 11 walitarajiwa kuondoka katika ndege ya Jumanne.

Hatahivyo, shirika la misaada la Care4Calais, ambalo lilikuwa ni miongoni mwa wale waliokata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya juu, lilisema kuwa watu wanane tu ndio wanaojiandaa kusafirishwa kwa ndege hadi Rwanda.

Idadi imepungua kwa kiwango kikubwa baada ya sera hiyo kupingwa kisheria ikihusishwa na utumwa wa kisasa na madai ya haki za binadamu, kilisema chanzo cha ndani cha Wizara ya mambo ya Ndani.

Serikali inatumaini kuwa mpango huo utawakatisha tamaa wanaoomba uhamiaji ya kuvuka njia za kuingia Uingereza na hivyo kuzuwia magenge ya wafanyabiashara haramu ya watu.

Lakini Care4Calais limeuelezea mpango huo kama " ukatili ", na mfumo huo umekosolewa na mashirika mengine, viongozi wa kidini navyama vya upinzani.

Sera hiyo itawasaidia watu hao kupata makazi na usaidizi nchini Rwanda huku maombi yao yakiangaliwa na serikali ya Rwanda.

Iwapo yatafanikiwa, wanaweza kuendelea kubakia nchini Rwanda kwa hadi miaka mitano, wakiwa na uwezo kupata elimu na usaidizi mwingine.

Wale ambao maombi yao ya uhamiaji yatakataliwa nchini Rwanda watapewa fursa ya kuomba kwa kutumia njia nyingine za uhamiaji, lakini wanaweza kukabiliwa nahatua ya kurejeshwa walikotoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live