Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaridhia mwanamke aliyemwacha mchumba aliyemsomesha apigwe faini

Couple Wachumba Mahakama yaridhia mwanamke aliyemwacha mchumba aliyemsomesha apigwe faini

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama nchini Uganda imetupilia mbali ombi la Fortunate Kyarikunda aliyetaka kubatilisha uamuzi wa faini ya Tsh. Ush10.4 Milioni (takriban Tsh. 6.2 Milioni) kwa kuvunja uchumba na kwa Richard Tumwine.

Mwezi uliopita Mahakama iligundua kuwa Fortunate alikiuka ahadi ya 2018 ya kuolewa na Richard aliyekuwa amemlipia ada ya kusomea diploma ya Sheria kwa makubaliano kwamba angemuoa hapo baadaye hivyo kupelekea Bw. Richard kufungua Shauri la madai kwa kupotezewa muda.

Richard aliiambia Mahakama kuwa mahusiano yao yalianza wakiwa Walimu wa Shule ya Msingi mnamo mwaka 2015, lakini Februari 2022 alibadilika na kuyavunja mahusiano kwa kigezo cha hawezi kuolewa na mzee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live