Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yamuachia Wenceslas Twagirayezu aliyetuhumiwa kwa mauaji ya Kimbari

Mahakama Yamuachia Wenceslas Twagirayezu Aliyetuhumiwa Kwa Mauaji Ya Kimbari Mahakama yamuachia Wenceslas Twagirayezu aliyetuhumiwa kwa mauaji ya Kimbari

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Mahakama inayoshughulikia kesi za mauaji ya kimbari nchini Rwanda imeamuru kuachilia huru Wenceslas Twagirayezu aliyetuhumiwa kwa mauaji ya kimbari.

Mahakama imesema hakuna ushahidi wa kutosha kutoka kwa mwendeshamashtakakwambaTwagirayezualikuwa nchini Rwandawakati mauaji ya kimbari yalipoanza April mwaka 94 .

Mahakama imeunga mkonohoja na ushahidi wa mtuhumiwa kwamba alikuwa katika nchi ya Zaire (ambayo sasa ni Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wakati mauaji ya kimbari yalipoanza nchini Rwanda.

Wenceslas Twagirayezu ndiye mtuhumiwa wa kwanza wa mauaji ya kimbari kutopatikana na hatia ya mauaji ya kimbari miongoni mwa watuhumiwa wa mauaji hayowaliopelekwa nchini Rwanda na nchi za kigeni hususan nchi za ulaya.

Twagirayezu ,56, alipelekwa nchini Rwanda na Denmark mwaka wa 2018 kufunguliwa mashitaka ya uhalifu wa mauaji ya halaiki.Kesi yake ilidumu kwa miaka 5.

Chanzo: Bbc