Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yakataa ombi la ANC kukifutia usajili chama cha Zuma

Mahakama Yakataa Ombi La ANC Kukifutia Usajili Chama Cha Zuma Mahakama yakataa ombi la ANC kukifutia usajili chama cha Zuma

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) kimeshindwa katika jitihada za kisheria kukizuia chama kipya ambacho kinaungwa mkono na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei.

ANC ilidai kuwa uMKhonto weSizwe, unaojulikana kama MK, haukuwa umekidhi vigezo vya usajili rasmi.

Mahakama ya uchaguzi nchini humo Jumanne asubuhi ilikataa pingamizi hilo.

ANC - ambayo kura ya maoni inatabiri inaweza kupoteza wingi wake wakati Waafrika Kusini watakapopiga kura tarehe 29 Mei - pia imeanzisha kesi tofauti za kisheria dhidi ya MK.

Chama kipya cha Bw Zuma kinapata umaarufu tangu alipojiunga nacho mapema mwaka huu, kura za maoni zinasema.

Jina la chama hicho linatokana na mrengo uliosambaratishwa wa ANC, ambao umekishutumu kwa ukiukaji wa hakimiliki.

Chanzo: Bbc