Mahakama ya Kenya dhidi ya ufisadi imekataa ombi la mwanawe Bw Kabuga Nshimyumuremyi Donatien kumruhusu mama yake kupata kodi ya nyumba katika mji mkuu, Nairobi, ripoti ya vyombo vya habari vya ndani.
Uamuzi huo ni kuthibitisha uamuzi wa Mahakama ya chini uliotolewa miaka 15 iliyopita.
Kesi hiyo, iliyowasilishwa mwaka wa 2008, ilitaka mali ya Bw Kabuga kupokonywa na mapato yake kutumika kuwafidia waathiriwa wa mauaji ya kimbari na familia zao.
Wakati huo, Bw Kabuga alikuwa ametoroka. Mkewe Bw Kabuga, katika mawasilisho yake aliyowasilisha mbele ya mahakama, alidai kuwa serikali ya Kenya haikuwa na uthibitisho kwamba mali iliyopingwa ilipatikana kupitia uhalifu.
Pia alidai kuwa hakuna uthibitisho kwamba Bw Kabuga alitumia kodi iliyokusanywa kutoka kwa nyumba hiyo ili kukwepa kukamatwa.
Bw Kabuga, mmoja wa washukiwa wakuu wa mauaji ya halaiki ya Rwanda mwaka 1994, alikamatwa nchini Ufaransa mwaka wa 2020 baada ya kukwepa kukamatwa kwa takriban miaka 26. Ameshtakiwa kwa makosa kadhaa ya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu.