Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaizuia Serikali kuwapeleka Polisi Haiti

Polisi Zi 800x500 Mahakama yaizuia Serikali kuwapeleka Polisi Haiti

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu nchini Kenya imezuia mipango ya serikali ya kupeleka maafisa wa polisi nchini Haiti au nchi nyingine yoyote ikisubiri kusikilizwa kwa ombi.

Jaji aliyetoa tamko hilo ametaja masuala yaliyoibuliwa katika maombi hayo kuwa yana umuhimu wa kitaifa na maslahi kwa umma. Mmoja wa walalamikaji aliyekuwa mgombeaji urais Ekuru Aukot amesema pendekezo hilo ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Aukot ameongeza kuwa nchi hiyo haina uwezo wa kuwaacha maafisa 1000 kwa ajili ya kutumwa Haiti kabla ya kushughulikia ukosefu wa usalama ndani ya taifa lao.

Wiki iliyopita mapigano ya kikabila magharibi mwa Kenya yalisababisha vifo vya watu saba na hivi karibuni eneo la pwani la Lamu limeshuhudia mashambulizi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab lenye uhusiano na Al-Qaeda lenye makao yake nchini Somalia, eneo hilo sasa liko chini ya amri ya kutotoka nje.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kenya amesisitiza kwamba mpango huo hautahatarisha usalama wa nchi kama ambavyo inasemwa na baadhi yao. Mahakama ya Kenya inatarajia kutoa maelekezo zaidi mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live