Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaidhinisha ushindi wa Rajoelina

Madagascar Ushindiiiii.jpeg Mahakama yaidhinisha ushindi wa Rajoelina

Sat, 2 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu ya Katiba ya Madagascar (HCC) jana Ijumaa ilipasisha ushindi wa rais aliyeko madarakani na kusema kuwa, kwamba Andry Rajoelina amechaguliwa tena kihalali kuwa rais wa Madagascar katika uchaguzi wa rais wa Novemba 16.

Tangazo hilo la jana la Mahakama Kuu ya Madagascar la kuunga mkono ushindi wa Rajoelina limekuja baada ya muungano wa upinzani Madagascar kusema kuwa hautayatambua matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 16 mwezi huu ambapo Andrey Rajoelina ametangazwa mshindi.

Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo, Rajoelina alipata asilimia 58.96 ya kura zilizopigwa, na kuvuka kiwango cha asilimia 50 kinachohitajika kushinda kwenye duru ya kwanza.

Mahakama Kuu ya Katiba ya Madagascar imesema katika taarifa yake ya jana kuwa, matokeo hayo ni sahihi licha ya kulalamikiwa na muungano wa upinzani.

Mahakama Kuu ya Madagascar imepasisha ushindi wa Rajoelina kwenye uchaguzi wa rais wa Novemba 16

Jumamosi iliyopita na Novemba 25, Tume ya Uchaguzi ya Madagascar ilitangaza kuwa Andry Rajoelina amepata ushindi wa kumuwezesha kuiongoza tena nchi hiyo kwa muhula wa tatu katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Rais uliosusiwa na karibu wagombea wote wa upinzani.

Tume hiyo ilitangaza kuwa, Rajoelina ameshindakwenye duru ya kwanza ya uchaguzi wa Rais hatua ambayo ilimfanya Andrey Rajoelina ajitokeze mbele ya vyombo vya habari mjini Antananaripo na kuwapongeza wananchi wa Madagascar kwa kumchagua tena kuliongoza taifa hilo linaloundwa na viisiwa kadhaa vya katika Bahari ya Hindi kikiwemo kisiwa kikubwa zaidi barani Afrika.

Alidai katika hotuba yake mbele ya waandishi wa habari kwamba, kwenye uchaguzi wa huo amepata zaidi ya kura milioni 2 na 850,000 jambo ambalo lisema, linalonyesha azma ya wananchi wa Madagascar ya kuendeleza njia ya maendeleo na ustawi wa nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live