Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yafutilia mbali mswada mzima wa BBI

D25fb4c4c83029f6 Mahakama yafutilia mbali mswada mzima wa BBI

Fri, 14 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mnamo Alhamisi, Mei 13, majaji watano wa mahakama kuu walitangaza kuwa mpango mzima wa maridhiano (BBI) ulikiuka katiba

- Mahakama kuu ilisema BBI ilianzishwa na Rais Uhuru Kenyatta binafsi ambapo kinyume na kifungu cha 257 cha katiba

- Aidha ilisema kwamba marekebisho katika katiba ni suala ambalo linapaswa kuamuliwa na wananchi

Waanzilishi wa marekebisho yaliyopendekezwa ya katiba kupitia mchakato wa maridhiano (BBI) wamepata pigo baada ya uamuzi wa kihistoria wa Mahakama Kuu uliotangaza mswada huo ni kinyume cha katiba.

Katika uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watano mnamo Alhamisi, Mei 13, mchakato wa BBI ulitangazwa kuwa haramu na uliokiuka katiba.

Majaji Joel Ngugi, George Odunga, Jairus Ngaah, Chacha Mwita na Teresia Matheka walisema BBI, iliyotokana na handisheki kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa Upinzani Raila Odinga, ilianzishwa na kiongozi wa taifa na ni kinyume na katiba.

"BBI ilikuwa mradi wa rais ambao ni kinyume na Kifungu cha 257 cha katiba. Jopo lililoteuliwa na rais Uhuru Kenyatta halikuwa na mamlaka ya kusimamia shughuli ya marekebisho ya katiba," majaji walisema.

Pia waliwalaumu waanzilishi wa BBI kwa kushindwa kutoa nakala za kutosha kwa umma wakiongeza kuwa wananchi wlaifungiwa nje licha ya katiba kuwaidhinisha kushiriki miswada ya aina hiyo.

Aidha majaji hao waliongeza kuwa Tume ya uchaguzi na mipaka IIEBC haikuwa na idadi ya kutosha ya makamishna kufanya uamuzi wowote unaoathiri sera kuu za taifa.

Majaji pia walikosoa pendekezo la BBI kubuni maeneo bunge mapya sabini wakishikilia kwamba jukumu hilo ni la tume ya uchaguzi na mipaka na sio la jopo lililoteuliwa na rais Kenyatta.

Jopo la majaji hao kwa kauli moja lilimsuta Uhuru na kudokeza kwamba alienda nje na mamlaka yake kwa kushinikiza kufanyia katiba marekebisho.

"Rais, serikali au chombo chochote cha serikali hakiwezi kushinikiza au kufanya maamuzi ya marekebisho katiba," korti ilisema.

Kwenye kura ya maoni ya BBI, korti iliamua marekebisho katika muswada wa katiba yanapaswa kupigiwa kura na wananchi.

"Muswada wa Marekebisho ya Katiba wa 2020 hauwezi kufanywa kwa kura ya maoni kabla ya IEBC kutekeleza zoezi la usajili wa wapiga kura katika nzima," sehemu ya uamuzi huo ilisema.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke