Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yafuta kesi za Ufisadi dhidi ya Washiriki wa Rais Ruto

Hukumu Pc Data Mahakama yafuta kesi za Ufisadi dhidi ya Washiriki wa Rais Ruto

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chini ya Serikali ya Rais mpya William Ruto, waendesha mashtaka wameondoa kesi kadhaa dhidi ya baadhi ya washirika wake kwa misingi sawa ya kesi hizo kukosa ushahidi

Kwa kuanzia, Novemba 10, 2022, Mahakama ilikubali ombi la Mwendesha Mashtaka la kuondoa kesi ya ufisadi ya Ksh. Bilioni 7.4 dhidi ya Naibu wa Rais Rigathi Gachagua, ikitaja ushahidi usiotosha.

Mnamo Mwezi Oktoba, DPP aliomba kuondoa mashtaka ya ufisadi dhidi ya Aisha Jumwa, ambaye sasa ni Katibu wa Baraza la Mawaziri, yanayohusiana na ubadhirifu wa Ksh. Milioni 19, pia aliondoa kesi dhidi ya aliyekuwa Gavana wa Kaunti ya Samburu Moses Lenolkulal, aliyeorodheshwa kwa nafasi ya Katibu Mkuu

Wakati huo huo, mnamo November 9, 2022, AishaJumwa alimtaka DPP kufutilia mbali kesi ya Mauaji dhidi yake, ambapo Katika kesi hiyo, anashtakiwa pamoja na Msaidizi wake kwa mauaji ya Bwana Ngumbao Jola wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Wabunge 2019

Chanzo: www.tanzaniaweb.live