Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaamuru washukiwa wa mauaji ya Shakahola wapatiwe matibabu

Pia Wewe Utakufa Siku Moja Mackenzie Amwambia Hakimu Mahakama yaamuru washukiwa wa mauaji ya Shakahola wapatiwe matibabu

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Mombasa nchini Kenya imeamuru mshukiwa mkuu wa mauaji ya Shakahola Paul Mackenzie na wengine 94 kupelekwa hospitali mara moja baada ya washukiwa hao kuwasili mahakamani wakiwa wamedhoofika kiafya.

Inasemekana washukiwa hao walikuwa wamesusia kula na kunywa maji kwa siku tatu. Hakimu Mkuu Alex Ithuku alilazimika kwenda kuwaona washukiwa hao katika eneo la kuegesha magari la mahakama ya Mombasa waliposhindwa kutembea na wengine wasiweze hata kufungua macho. Upande wa mashtaka hata hivyo umepinga kukubaliwa kwa ombi la washukiwa hao kuachiliwa kwa dhamana.

Wamedai kuwa kwa sasa ni hatari washukiwa hao kuachiwa kwani haitakuwa rahisi kuwapata au kujua wanakoishi na pia wanahofia wanaweza kutoweka na kukwepa adhabu ya mashtaka yanayowakabili. Kesi hii itatajwa tarehe 5 Machi, mwaka huu wakati mahakama itakapopanga tarehe ya kutoa uamuzi wa ombi la upande wa mashtaka la kupinga dhamana. Maafisa wakitoa miili ya wahanga wa sakata la Shakahola

Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma nchini Kenya, (ODPP) ilitangaza mwezi uliopita kwamba imefanikiwa kupata ushahidi wa kutosha wa kuwashtaki washukiwa 95 wa mauaji ya Shakahola katika kaunti ya Kilifi eneo la Pwani.

Shakahola ni eneo la msitu linalopatikana huko Malindi katika Kaunti ya Kilifi, ambapo mhubiri tata wa Kikristo mwenye misimamo mikali, Kasisi Paul Nthenge Mackenzie alikuwa akiendesha shughuli zake pamoja na wafuasi wake.

Anasemekana kuhimiza wafuasi wake kufunga kula na kunywa ili waage dunia ili eti waende kumuona Nabii Isa (Yesu). Idadi kubwa ya wafuasi wa kanisa hilo walipoteza maisha kwa kufuata agizo hilo.

Mackenzie na wafuasi wake kadhaa walikamatwa mwaka jana mwezi Aprili na wamekuwa kizuizini tangu wakati huo ili kutoa nafasi kwa uchunguzi. Miili ya watu 429 wakiwemo watoto imefukuliwa kutoka maeneo ya makaburi huko Shakahola na uchunguzi umebaini kuwa mbali na kufa njaa wengine wakibainika kupoteza maisha kupitia kunyongwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live