Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaamuru kukamatwa kwa seneta wa Nakuru Tabitha Karanja

Mahakama Yaamuru Kukamatwa Kwa Seneta Wa Nakuru Tabitha Karanja Mahakama yaamuru kukamatwa kwa seneta wa Nakuru Tabitha Karanja

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mahakama ya Nairobi imetoa kibali cha kukamatwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Keroche Tabitha Karanja kwa kukosa kuhudhuria kusikilizwa kwa kesi yake ya malipo ya ushuru ya Sh14.5 bilioni.

Hakimu mkuu mwandamizi wa Milimani Esther Kimilu alitoa kibali hicho baada ya mahakama kuambiwa kuwa Seneta wa Nakuru hakuwepo katika kesi yake.

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama kutoa kibali na kupanga kusikizwa kwa kesi hiyo Alhamisi asubuhi.

Kesi hiyo itaendelea kesho Tabitha anatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Mnamo Aprili, Tabitha alishtakiwa upya na alikana mashtaka 10 ya kukwepa kulipa ushuru.

Hii ilikuwa baada ya upande wa mashtaka kuomba kurekebisha mashtaka, akisema baadhi ya maelezo hayapo kwenye karatasi ya mashtaka ya 2019.

Kwa mujibu wa shtaka hilo, washtakiwa na kampuni hiyo katika tarehe kati ya Februari 20, 2015 na Januari 20, 2016, kinyume cha sheria walitoa taarifa zisizo sahihi katika marejesho ya ushuru kwa kupunguza ushuru kwa Sh1.8 bilioni.

Alidaiwa pia kutoa taarifa zisizo sahihi za marejesho ya Januari hadi Desemba 2017, ambayo yaliathiri ushuru wa Sh3.6 bilioni.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, kati ya Februari 20 na Julai 20, washtakiwa waliacha kurudisha VAT kwa Januari hadi Juni kinyume cha sheria na kuathiri dhima yao ya VAT kwa Sh196 milioni.

Tabitha pia alishtakiwa kwa kutangaza chini ya kiwango cha uzalishaji kwa lita 820,601 na matumizi mabaya ya viwango vya ushuru wa bidhaa kwenye Vienna Ice kwa kutumia Sh27.06 badala ya Sh175, na hivyo kupunguza dhima yake ya ushuru kwa Sh1, 855, 403, 900 inayolipwa kwa kamishna kama inavyotakiwa na Sheria ya Ushuru wa Bidhaa.

Hata hivyo upande wa utetezi uliitaka mahakama kuwa wanataka kusuluhisha suala hilo nje ya mahakama.

"Tayari tumeanzisha mchakato wa kusuluhisha suala hilo na KRA na ikiwa mahakama inaruhusu, tunataka suala hilo kusuluhishwa," mahakama iliambiwa.

Mwakilishi wa KRA ambaye alikuwepo kortini alisema afisi hiyo haina nia ya kusuluhisha suala hilo nje ya mahakama kwa kuwa hawajapokea taarifa zozote.

Chanzo: Radio Jambo