Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yaamuru Rais Zuma akamatwe

94426 Zumac+pic Mahakama yaamuru Rais Zuma akamatwe

Wed, 5 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Johannesburg, Afrika Kusini. Mahakama ya juu ya Pietermaritzburg nchini Afrika Kusini imetoa hati ya kukamatwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumanne Januari 4 baada ya kiongozi huyo kushindwa kufika mahakamani hapo kukabiliana na mashtaka ya rushwa yanayomkabili.

Hata hivyo, hati hiyo itafanya kazi iwapo atashindwa kuhudhuria kesi yake iliyopangwa kufanyika mwezi Mei.

Rais Zuma anakabiliwa na makosa 16 ya kughushi, rushwa, ulaghai na utakatishaji fedha ukihusisha biashara ya silaha yeye thamani ya mabilioni ya dola iliyofanywa miaka ya 1990.

Awali jopo la wanasheria wake waliwasilisha nyaraka mahakamani hapo wakieleza kuwa  mteja wao ni mgonjwa na amekuwa akipatiwa matibabu nje ya Afrika Kusini tangu mwezi uliopita.

Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa na Jaji Dhaya Pillay ambaye alihoji maelezo yaliyo kwenye nyaraka za matibabu za Rais Zuma zilizowasilishwa na mawakili wake mahakamani na kutoa hati ya kumkamata iwapo hatoweza kuhudhiria kesi hiyo itakapokuja tena mwezi Mei.

Pia Soma

Advertisement
Raia huyo wa zamani pia anakabiliwa na tuhuma za rushwa ikihusisha malipo 783 yenye utata anayodaiwa kupokea kutoka kwa aliyekuwa mshauri wake wa masuala ya fedha, Schabir Shaik.

Madai hayo pia yamerejelea mkataba wa silaha uliofanyika miaka ya 1990 na kampuni moja ya masuala ya ulinzi ya nchini Ufaransa.

Chanzo: mwananchi.co.tz