Raia 32 wa Kenya wamehukumiwa kifungo cha mika 10 na mahakma ya kijeshi yenye makao yake katika wilaya ya kaskazini mwa Uganda ya Moroto.
Naibu msemaji wa jeshi la Uganda Kanali Deo Akiiki amethibitisha taarifa hii.
Walipatikana na hatia ya kumiliki sbunduki na risasi kinyume cha sheria, makosa yanayoshitakiwa katika Mahakama ya kijeshi nchini Uganda.
Kila kosa linapelekea kifungo cha miaka 10 jela. Mahakamailiamuru Jumatano kuwa watatakiwa kutumikia kifungo kwa wakati mmoja.
Wakenya hao wote ni wakazi wa kaunti ndogo ya Orum ilitopo katika wilaya ya Lodwar, katika Kaunti ya Turkana na walipatikana na hatia baada ya kukiri wenyewe. Watatumikia kifungo hicho katika gereza la serikali la Moroto.
Walikuwa ni miongoni mwa washikiwa zaidi ya 100 waliokamatwa tarehe 8 Aprili kutoka kwenye maficho yao katika kijiji cha Lokeriaut kilichopo katika kaunti ndogo ya Nanduget wilayani Moroto Uganda.
Jeshi limepata bunduki haramu 31 na risasi zipatazo 751 wakati wa operesheni ambayo ni sehemu ya zoezi la msako wa kuwapokonya silaha watu wanaozimiliki kinyume cha sheria.