Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya juu kusikiliza rufaa dhidi ya ugombea urais wa Zuma

Jacob Zuma Aondolewa Hukumu Ya Kifungo Cha Miaka 15 Yaondolewa Mahakama ya juu kusikiliza rufaa dhidi ya ugombea urais wa Zuma

Fri, 10 May 2024 Chanzo: Bbc

Mahakama ya juu nchini Afrika Kusini inajiandaa kusikiliza rufaa kuhusu iwapo rais wa zamani Jacob Zuma atastahili kugombea katika uchaguzi unaotabiriwa kuwa karibu.

Bw Zuma, 82, anaongoza chama kipya cha upinzani, Umkhonto we Sizwe (MK) chama, ambacho wachambuzi wanasema kinaweza kuvuruga matokeo ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Mei.

Mnamo Aprili Mahakama ilisema kwamba alikuwa huru kugombea baada ya tume ya uchaguzi kumzuia kwa kupuuza hukumu ya mahakama.

Ilikuwa imedai kuwa katiba inawazuia watu kushikilia ofisi ya umma ikiwa watapatikana na hatia ya uhalifu na kuhukumiwa kifungo cha zaidi ya maka mmoja jela.

Bw Zuma alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela mwaka wa 2021 kwa kukosa kutoa ushahidi katika uchunguzi wa ufisadi, na alitumikia kifungo hicho kwa miezi mitatu kabla ya kuachiwa kwa misingi ya kiafya.

Chanzo: Bbc