Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya juu Nigeria kutoa uamuzi kuhusu pingamizi la kura ya urais

Mahakama Ya Juu Nigeria Kutoa Uamuzi Kuhusu Pingamizi La Kura Ya Urais Mahakama ya juu Nigeria kutoa uamuzi kuhusu pingamizi la kura ya urais

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama ya Juu zaidi ya Nigeria inatazamiwa kutoa uamuzi kuhusu iwapo itaunga mkono au kutounga mkono ushindi wa rais Bola Tinubu ambao ulikuwa na utata katika uchaguzi.

Wapinzani wake wawili wakuu, Atiku Abubakar wa Peoples Democratic Party na Peter Obi wa Labour Party, wanatafuta kubatilisha uchaguzi wa urais wa Februari, kwa madai kuwa ulikumbwa na kasoro.

Mahakama ya Juu ilikuwa na siku 60 kutoa uamuzi wake. Lakini imeamua kuharakisha uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za wapinzani Jumatatu.

Bw Abubakar alitoa ushahidi mpya, akisema cheti ambacho Rais Tinubu aliwasilisha kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi kinatofautiana na kile kinachodaiwa kutolewa na Chuo Kikuu cha Jimbo la Chicago.

Mpinzani mwingine, Bw Obi, alisema kuwa Bw Tinubu hakuwa na sifa za kuwania urais wa Nigeria wakati huo.

Wanasisitiza kuwa mahakama ya juu zaidi nchini inafaa kubatilisha uamuzi wa Mahakama ya Malalamiko ya Uchaguzi, ambayo iliidhinisha ushindi wa Bw Tinubu mwezi uliopita.

Iwapo itaunga mkono uamuzi wa mahakama ya chini, hiyo itakuwa ni kufuata mtindo ulioonekana katika chaguzi zilizopita katika taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika, ambapo matokeo ya uchaguzi wa urais hayajawahi kubatilishwa.

Chanzo: Bbc