Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya Zimbabwe Yabatilisha Uamuzi wa Rais Mnangagwa

Jaji?fit=800%2C450&ssl=1 Mahakama ya Zimbabwe Yabatilisha Uamuzi wa Rais Mnangagwa

Mon, 17 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mahakama ya Zimbabwe Yabatilisha Uamuzi wa Rais Mnangagwa May 17, 2021 by Global Publishers



Mahakama Kuu nchini Zimbabwe, jana ilitangaza kuwa, uamuzi wa Rais Emmerson Mnangagwa kumuongezea muda Jaji Mkuu wa nchi hiyo ni kinyume cha sheria.

Wiki iliyopita, Mnangagwa alitangaza habari ya kumuongezea muda Luke Malaba wa kuwa jaji mkuu wa Zaimbabwe kwa muda wa miaka mitano zaidi. Hatua hiyo ilikuja masaa machache kabla ya Jaji Mkuu huyo kumaliza muda wake wa kushikilia cheo hicho kwa mujibu wa sheria.

Majaji wa Mahakama Kuu jana walisema kuwa, Malaba aliacha kuwa Jaji Mkuu wa Zimbabwe kuanzia jana tarehe 15 Mei, 2021 na kwamba hatua ya Rais Mnangagwa ya kumuongezea muda Malaba ni kinyume cha katiba.

Malaba analaumiwa kwa kuipendelea serikali ya Mnangagwa. Alidharau kusikiliza kesi ya kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa ya kulalamikia uchakachuaji wa kura za urais katika uchaguzi wa mwaka 2018.

Baada ya Mahakama Kuu ya Zimbabwe kubatilisha uamuzi huo wa Rais mnangagwa, wizara ya sheria na masuala ya bunge ya nchi hiyo imetoa taarifa na kusema itakata rufaa ikilalamika kwamba Mahakama Kuu ya Zimbabwe imetekwa na nguvu za wageni na maadui wa taifa la Zimbabwe.

Kabla ya kutangaza kurefusha muda wa Jaji Mkuu, Mnangagwa alitia saini sheria ya mabadiliko ya katiba yanayompa nguvu zaidi Rais wa Zimbabwe katika uteuzi wa majaji. Hatua hiyo ya bunge la Zimbabwe ililalamikiwa vikali, lakini Mnangagwa alitia saini muswada huo na kuufanya kuwa sheria.

Chanzo: globalpublishers.co.tz