Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya Rwanda yamzuia kiongozi wa upinzani kuwania urais

Mahakama Ya Rwanda Yamzuia Kiongozi Wa Upinzani Kuwania Urais Mahakama ya Rwanda yamzuia kiongozi wa upinzani kuwania urais

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Mahakama kuu katika mji mkuu wa Rwanda Kigali imetupilia mbali ombi la kiongozi maarufu Victoire Ingabire kutaka kurejeshewa haki zake zote za uraia ambazo zitamruhusu kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi Julai.

Bi Ingabire aliwaambia waandishi wa habari nje ya mahakama kwamba mahakama ya Rwanda "iko mbali na uhuru" ikiwa sheria ya juu (katiba) ilimpa haki, "lakini jaji leo aliegemeza uamuzi wake juu ya amri ya rais".

Bi Ingabire ambaye amefungwa kwa miaka minane na kusamehewa na Rais Paul Kagame mwaka 2018 kabla ya kukamilisha kifungo chake cha miaka 15, alitarajia kushindana na rais katika uchaguzi ujao.

"Sikubaliani na kile jaji alisema, na kwa bahati mbaya huwezi kukata rufaa kabla ya miaka miwili ... Bado tuko mbali na nchi inayotii sheria" aliwaambia waandishi wa habari.

Chanzo: Bbc