Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya Rufaa Kenya: Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kiwango (SGR) Ulikuwa Haramu

SGR KENYA Mahakama ya Rufaa Kenya: Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kiwango (SGR) Ulikuwa Haramu

Thu, 2 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Rufaa nchini Kenya imesema kuwa mkataba wa makubaliano kati ya Shirika la Reli Kenya na kampuni ya China Bridges and Railway Corporation (CRBC) ulifanyika bila kufuata mchakato wa manunizi ya umma, ushindani na sheria za Kenya, umeripoti mtandao wa International Railway Journal

Hukumu hiyo imepindua hukumu iliyotupilia mbali kesi hiyo iliyotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2014, Isaac Lenaola ambaye kwasasa anahudumu katika Mahakama ya Rufaa.

Mahakama ya Rufaa imeamua kuwa Shirika la Reli la Kenya halikufuata Ibara ya 227 (1) ya katiba ya Kenya inayotaka taasisi za umma kufanya manunuzi ya huduma na bidhaa katika namna ambayo ni ya ‘’haki, uwazi, usawa, ushindani na kuzingatia unafuu wa gharama’’

Vilevile, majaji wamesema kuwa Shirika la Reli lilikiuka sheria za ugavi na manunuzi za nchi hiyo. Shirika hilo lilikiuka kifungu cha 29 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma yam waka 2005, ambayo inalenga kuhakikisha kuwa kunakuwa na mchakato wa wazi wa kuwapata wazabuni kwenye taasisi za umma, ikiwamo shirika la reli kulinda usawa wa ushindani katika mchakato wa kumpata mzabuni.

Hukumu hiyo imekuja kwa kuchelewa ambapo reli kutoka Mombasa, hadi Nairobi na Naivasha imeshakamilika na kuanza kutumika ikigharimu fedha za Kenya shilingi bilioni 314.2 kukamilisha ujenzi. Hata hivyo, hukumu hiyo imeongeza shaka kuhusu uhalali wa deni ambalo kampuni mama ya CBRC ya China Communications Construction Company (CCCC) inaidai Kenya na pia nafasi ya CCCC katika kuendesha reli hiyo huko mbeleni.

Ujenzi wa reli hiyo yenyen urefu wa Kilomita 480 za reli ya kiwango ulifanyika kama mbadala wa reli nyembamba ya mita moja iliyojengwa mwaka 1901 na wakoloni. Ujenzi wa urefu uliobaki kuelekea kwenye mpaka na Uganda wa Malaba ulipangwa kuanza Julai 2019, ingawa hadi sasa haujaanza na serikali ya taifa hilo iliamua kufanya ukarabati na uboreshaji wa reli ya upana wa mita na kuiunganisha na reli mpya ya kiwango (SGR).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live