Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya Kikatiba DR Congo yasema haina sifa kumhukumu Waziri Mkuu

Matata Ponyo Senat 21 01.jpeg Mahakama ya Kikatiba DR Congo yashindwa kumhukumu Waziri Mkuu Matata Ponyo

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa haina uwezo wa kumhukumu aliyekuwa Waziri Mkuu Augustin Matata Ponyo.

Mahakama ya juu zaidi nchini DRC imesema leo Jumatatu (Novemba 15) kwamba haina uwezo wa kumhukumu aliyekuwa waziri mkuu Seneta Augustin Matata Ponyo. Seneta mteule wa bunge la sasa, Augustin Matata Ponyo anashutumiwa kwa ubadhirifu wa mamia ya mamilioni ya dola zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa bustani ya kilimo ya Bukanga-Lonzo.

Katika kesi hiyo, watu wengine wawili pia wanashitakiwa: Patrice Kitebi, Waziri wa zamani wa Fedha, na Kristo Groblert, meneja wa kampuni ya Africom ya Afrika Kusini.

Wiki moja iliyopita, upande wa utetezi wa Matata Ponyo ulionyesha kwa jinsi gani Mahakama ya Kikatiba haina uwezo wa kumhukumu.

Kinachobaki sasa ni upande wa serikali kufahamu itafanya nini na inakusudia vipi kupata suluhu na ni mahakama gani itakayopewa mamlaka ya kuwahukumu washtakiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live