Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya Kenya yazuia tozo mpya ya vitambulisho

High Court Kenya1552639686968 AspR 1 Mahakama ya Kenya yazuia tozo mpya ya vitambulisho

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama Kuu ya Kenya imezuia tozo mpya ya vitambulisho vya taifa ambayo ilikuwa imezua gumzo kali.

Ombi la daktari wa upasuaji Magare Gikenyi lilisema kuwa serikali iliwasilisha tozo hiyo kwa "njia isiyo na msingi na ya kiholela".

Ombi hilo lilisema kuwa tozo hiyo itawazuia "raia wa kawaida" kupata vitambulisho vya kitaifa.

Vitambulisho vilikuwa vikitolewa bila malipo lakini ada ya shilingi 1,000 za Kenya ($6; £5) ilianzishwa bila maelezo yoyote.

Gharama ya kubadilisha vitambulisho pia imeongezeka mara 20 hadi shilingi 2,000.

Wakenya tayari wanajitahidi kukabiliana na gharama ya maisha, na kuanzishwa, au kuongezwa kwa malipo tofauti huku serikali, ikijaribu kuongeza mapato yake.

Baadhi ya wamelalamikia malipo ya juu zaidi kwa huduma za serikali ambazo wanaamini tayari zinafadhiliwa na kodi wanayolipa.

Chanzo: Bbc