Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya Juu ya Nigeria imetupilia mbali pingamizi dhidi ya Rais Bola

Mahakama Ya Juu Ya Nigeria Imetupilia Mbali Pingamizi Dhidi Ya Rais Bola Mahakama ya Juu ya Nigeria imetupilia mbali pingamizi dhidi ya Rais Bola

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama ya Juu nchini Nigeria imetupilia mbali pingamizi zote mbili za upinzani dhidi ya ushindi wa Rais Bola Tinubu.

Wagombea hao wawili wakuu wa upinzani walikuwa wanataka kutengua uchaguzi wa urais wa Februari, kwa madai kuwa ulikumbwa na kasoro.

Mahakama ya Malalamiko ya Uchaguzi iliidhinisha ushindi wa Bw Tinubu mwezi uliopita, lakini upinzani ulisisitiza kuwa mahakama ya juu zaidi ya Nigeria inapaswa kufuta uamuzi huo.

Matokeo ya uchaguzi wa rais hayajawahi kubatilishwa nchini Nigeria.

Majaji hao kwanza walitupilia mbali pingamizi lililotolewa na Atiku Abubakar, ambaye aliibuka wa pili katika uchaguzi huo, na kisha kulikataa la Peter Obi, ambaye aliibuka wa tatu.

Uchaguzi huo ulikuwa wenye ushindani mkali zaidi tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka wa 1999, na wagombea watatu wenye nguvu kwa mara ya kwanza.Bw Tinubu alishinda kwa 37% ya kura zilizopigwa, dhidi ya 29% za Bw Abubakar na 25% za Bw Obi.

Chanzo: Bbc