Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya Juu Nigeria yasitisha tarehe ya mwisho kubadilisha noti

Mahakama Ya Juu Yasitisha Tarehe Ya Mwisho Kubadilisha Noti Mahakama ya Juu Nigeria yasitisha tarehe ya mwisho kubadilisha noti

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama ya Juu Zaidi nchini Nigeria imesitisha kwa muda makataa ya Ijumaa ya kuacha kutumia noti za zamani, jambo ambalo lilikuwa limesababisha mzozo wa fedha nchini humo.

Benki nyingi hazijapata noti mpya za naira za kutosha, na kusababisha matukio ya kukata tamaa na machafuko huku watu wakijaribu kuzipata.

Video zilitolewa za watu wakivua nguo kwenye benki katika maandamano na mapigano kwenye ATM.

Machafuko hayo yalisababisha wasiwasi kuwa huenda yakaathiri uchaguzi wa mwezi huu, kwani Wanigeria wengi hawana akaunti za benki.

Benki Kuu ilitangaza sarafu iliyobuniwa upya katika jaribio la kudhibiti mfumuko wa bei, ambao kwa sasa unaendelea kwa 20%.

Kesi hiyo iliyoletwa na majimbo ya kaskazini ya Kaduna, Kogi na Zamfara imeahirishwa hadi Februari 15.

Chanzo: Bbc