Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya Juu Kenya yaamua wapenzi jinsia moja wanayo haki kujumuika

Mahakama Ya Juu Kenya Yaamua Wapenzi Jinsia Moja Wanayo Haki Kujumuika Mahakama ya Juu Kenya yaamua wapenzi jinsia moja wanayo haki kujumuika

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Juu ya Kenya imeamua kwamba uamuzi wa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwazuia wapenzi wa jinsia moja kuunda vikundi vinavyotambulika ni ya kibaguzi.

Mahakama ilisema kuwa licha ya mapenzi ya jinsia moja yameharamishwa nchini Kenya, wanachama wa LGBTQ bado wana haki ya kujumuika.

Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Jaji Smokin Wanjala na Jaji Njoki Ndung’u walitoa uamuzi katika upande wa wengi kuhusu suala hilo.

Jaji Mohamed Ibrahim na William Ouko walipinga, wakisema kwamba wapenzi wa jinsia moja hawafai kuruhusiwa kuunda vyama vinavyotambulika nchini Kenya.

Uamuzi huo sasa unawapa wapenzi wa jinsia moja uwezo wa kutafuta kutambuliwa rasmi na Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Mnamo Novemba 23, 2021 Mahakama ya Juu ilisikiliza kesi ya kupinga maamuzi ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa ya kuruhusu Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu za wapenzi wa jinsia mojanchini Kenya (NGLHRC) kusajiliwa rasmi kama shirika lisilo la kiserikali (NGO).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live