Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya DRC yamhukumu mwanahabari kifungo cha miezi sita jela

Mahakama Ya DRC Yamhukumu Mwanahabari Kifungo Cha Miezi Sita Jela Mahakama ya DRC yamhukumu mwanahabari kifungo cha miezi sita jela

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Mahakama ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumatatu ilimpata mwandishi wa habari wa Congo Stanis Bujakera na hatia ya kueneza habari za uongo miongoni mwa mashtaka mengine, na kumhukumu kifungo cha miezi sita jela, wakili wake alisema.

"Majaji walimkuta mteja wetu na hatia ya mashtaka yote kama ilivyothibitishwa.

Wametoa adhabu kali zaidi ya miezi 6, pamoja na kulipa faini ya faranga milioni 1 za Congo ($364)," wakili wa Bujakera, Jean-Marie Kabengela, aliwaambia waandishi wa habari.

Aliongeza kuwa Bujakera, ambaye anafanya kazi katika vyombo vya habari vya kimataifa ikiwa ni pamoja na Jeune Afrique na Reuters, anatarajiwa kuondoka katika gereza ambalo amekuwa akishikiliwa tangu Septemba mwaka jana Jumanne kwa sababu tayari ameshatumikia muda huo.

Wakili huyo alisema, kwa kuzingatia taratibu za kawaida katika kesi hizo, timu ya mawakili inayomwakilisha Bujakera itarejea tena mahakamani hapo Jumanne, kupata nakala ya uamuzi huo na kulipa faini hiyo ili aachiliwe.

Bujakera, ambaye amekana mashtaka yote, alikamatwa katika mji mkuu Kinshasa kwa tuhuma za kueneza habari za uongo kuhusu mauaji ya mwanasiasa mashuhuri wa upinzani katika makala iliyochapishwa na Jeune Afrique, gazeti la habari la Ufaransa limesema.

Mwendesha mashtaka katika kesi hiyo mapema mwezi huu alikuwa ameitaka mahakama ya Kinshasa kumhukumu Bujakera kifungo cha miaka 20 jela.

Mashirika ya haki za ndani na kimataifa yakiwemo Reporters Without Borders na Amnesty International yalilaani kuzuiliwa kwa Bujakera, na kuliita shambulio dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari.

Reuters pia imetoa wito wa kuachiliwa kwake.

Chanzo: Bbc