Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama ya DR Congo imethibitisha ushindi wa Tshisekedi

Mahakama Ya DR Congo Imethibitisha Ushindi Wa Tshisekedi Mahakama ya DR Congo imethibitisha ushindi wa Tshisekedi

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Kikatiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetupilia mbali mapingamizi mawili ya kisheria dhidi ya matokeo ya muda ya uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi uliopita na kumtangaza Rais Félix Tshisekedi kuwa mshindi wa mwisho.

Bw Tshisekedi alipata 73.47% ya kura, mahakama ilisema.

Mahakama iliidhinisha ushindi wa kiongozi huyo licha ya ripoti za waangalizi huru kuhusu dosari zilizoenea wakati wa kura ya Disemba 20.

Uchaguzi huo pia ulikumbwa na matatizo mengi ya vifaa, ambayo upinzani ulisema ni sehemu ya mpango wa makusudi wa kuchakachua matokeo ili kumpendelea Bw Tshisekedi.

Ni mgombea mmoja tu wa upinzani kati ya kumi na wanane aliyepeleka suala hilo mahakamani.Wengine akiwemo mshindi wa pili, Moïse Katumbi, alikataa kuwasilisha pingamizi la kisheria baada ya kutilia shaka uhuru wa mahakama.

Mahakama ya Kikatiba iliamua Jumanne kwamba kasoro zilizoripotiwa hazingeweza kuathiri matokeo ya uchaguzi kwa sababu kulikuwa na pengo kubwa kati ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo na Bw Katumbi, ambaye alipata takriban 18% ya kura.

Uamuzi huo umefungua njia kwa Bw Tshisekedi kuapishwa kwa muhula wa pili tarehe 20 Januari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live